Sengerema FM

Mavunde awatuliza wananchi mgodi wa Sota Sengerema

13 October 2024, 12:01 pm

Waziri wa Madini Mh,Anton Mavunde akizungumza na wananchi eneo la SOTA lililopo Sengerema.Picha na Emmanuel Twiamnye

Mgodi wa dhahabu wa SOTA GOLD Mining uliopo kata ya Igalula wilayani Sengerema mkoani Mwanza unatarajiwa kuanza uzalishaji mwakani 2025, ambapo kwasasa wameaanza madalizi ya ujenzi wa Mgodi huo,ikiwemo kuwahamisha wananchi wenye maeneo yanayo pakana na eneo la mgodi huo.

Na;Emmanuel Twimanye

Wananachi Waliopisha Mgodi wa Sotta  uliopo katika Kijiji cha Sota kata ya Igalula Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza  wameiomba Serikali kuingilia kati suala la kujengewa nyumba   sambamba na wazawa kupewa kipaumbele cha ajira katika mgodi huo.

Wananchi hao wametoa ombi hilo  mbele ya wazairi wa madini  Mh,Anton Mavunde  katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ngoma.

Sauti za wananchi wakizungumzia changamoto zao kwa waziri wa madini Mh. Antony Mavunde

Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh, Hamis Tabasam  amewaomba viongozi wa kampuni hiyo ya mgodi kuhakikisha wanajenga nyumba za  wanufaika haraka huku akimuomba waziri kuhakikisha mgodo huo unatenga eneo ala wachimbaji wadogo.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh, Hamis Tabasam akizungumzia changamoto za wananchi wa Sota

Afisa Mkuu wa Fedha na kaimu meneja wa Mgodi wa Sota  Isack  Lupokela  amesema kuwa tayari wakandarasi wamekwisha patikana kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo pamoja na  kuahidi kulipa kipaumbele suala la ajira kwa wazawa. 

Sauti ya Afisa Mkuu wa Fedha na kaimu meneja wa Mgodi wa Sota  Isack  Lupokel akizungumzia namna wanavyotatua changamoto za wananchi

Naye  Waziri wa Madini Mh,Anton Mavunde amemwagiza Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Nganga  kuhakikisha anasimamia zoezi la ajira kikamilifu ili wazazwa waweze kunufaika na mgodi huo.

Sauti ya Waziri wa Madini Mh,Anton Mavunde akizungumza na wananchi wa Sota