Sengerema FM

Jamii yatakiwa kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu

12 October 2024, 5:20 pm

Mwanafunzi Mussa Malingo akiwa kwenye baiskeli mwendo aliyokabidhiwa na shirika la SMD.Picha na Joyce Rollingstone

Shule ya msingi Tabaruka iliyopo halmashauri ya Sengerema ni miongoni mwa shule zinazofundisha watoto wenye ulemavu Sengerema huku ikikabiliwa na changamoto ya vitendea kazi au vifaa wezeshi kwa watoto hao.

Na Joyce Rollingstone

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Sengerema Mshikamano on Disability SMD lililopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza, limemkabidhi baiskeli mtoto mwenye ulemavu wa viungo katika shule ya msingi Tabaruka.

Akikabidhi baiskeli hiyo Mkurugenzi wa Shirika hilo Bwn Gervas Titus, amesema kuwa  baiskeli hiyo wameitoa kwa ajili ya mtoto Musa Malingo mwenye ulemavu wa viungo, anayesoma katika shule hiyo hatua ya awali.

Sauti ya Mkurugenzi wa Shirika hilo Bwn Gervas Titus akihimiza kuitunza baiskeli iliyotolewa kwa mtoto Mussa Malingo

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwn Ramadhani Kisinza Joseph, amelipongeza shirika hilo kwa kumsaidia mtoto  huyo na kusema kuwa itamsaidia kufika shuleni kwa wakati ikiwa ni pamoja  na kuwaomba waendelee kuwasaidia na wengine wenye mahitaji kama hayo.

Sauti ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwn Ramadhani Kisinza Joseph, akilipongeza shirika hilo la SMD kwa kutoa msaada huo

Akipokea baiskeli hiyo mzazi wa mtoto huyo Bwn Jemsi Malingo Stephano,amelishukuru Shirika hilo ,huku akiahidi kuitunza na kuhakikisha inatumika kwa matimizi ya mtoto huyo, huku  kubainisha changamoto alizokuwa akuzipitia hapo awali.

Sauti ya Mzazi wa mtoto huyo Bwn Jemsi Malingo Stephano akiahidi kuitunza baiskeli hiyo

Naye Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Tabaruka Bwn Dickson Denis, ametoa wito kwa Wazazi na Walezi kuhakikisha mtoto mwenye ulemavu anapata haki zake za msingi ikiwemo Elimu na atakaye kiuka kumpeleka mtoto Shule hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Sauti ya Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Tabaruka Bwn Dickson Denis akiwataka wazazi kuwapeleka watoto wenye ulemavu shule

Makabidhiano hayo yamefanyika katika shule ya msingi tabaruka na kuhudhuliwa na walimu,mzazi ,viongozi wa selikari pamoja na viongozi wa shirika la Sengerema Mshikamano On Disability SMD.