Mzava akemea vitendo vya rushwa uchaguzi serikali za mitaa
9 October 2024, 1:13 pm
Mwenge wa uhuru mwaka huu katika Halmashauri ya Sengerema umefanikiwa kuifikia miradi sita yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 4.6
Na: Jovna George
Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa amewataka wananchi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza kushirikiana kwa pamoja kutokomeza vitendo vya rushwa hususani katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Akizungumza na wananchi Wilayani Sengerema kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndg Godfray Eliakimu Mzava katika uwanja wa Tabasamu Stadium amewataka watanzania kuepukana na vitendo vya rushwa hasa kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa ili kupata viongozi wenye uwezo wa kuwaletea maendeleo na kuwaongoza.
Kiongozi huyo amesema kuwa kila mmoja anapaswa kutoa taarifa sehemu husika endapo atabaini vitendo viovu vya uvunjifu wa Amani sambamba na ulimaji pamoja na uvutaji wa bangi ili kuondokana na athari zinazosababishwa ba utumiaji wa madawa ya kulevya.
Hata hivyo Mzava amewakumbusha wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi utakao fanyika tarehe 27/11/2024 na kupiga kura kuwachagua viongozi wenye sifa za kuwatumikia.