Wazazi watakiwa kuwalinda watoto waliohitimu darasa la 7
9 October 2024, 12:55 pm
Shule ya Msingi Matwiga ni miongoni mwa Shule mpya za msingi zilizojengwa katika kata ya Mission halmashauri ya Sengerema
Na;Jovna George
Diwani wa kata ya misheni Wilayani Sengerema Francis Mbungai amewataka wazazi na walezi kuwalinda watoto waliohitimu Darasa la saba wakati wakisubiri matokeo ya mtihani ili waweze kutimiza ndoto zao za kielimu.
Hayo yamesemwa na Diwani huyo katika mahafali ya Darasa la sba katika shule ya Msingi Matwiga na kusema kuwa wazazi na walezi watakao washawishi watoto wao kuolewa ama kufanya kazi za nyumbani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Vile vile Wazazi wamewasihi wahitimu wa darasa la saba kuepuka vishawishi mitaani na kuzingatia walichokipata shule ili kufikia malengo yao.
Awali Wakisoma lisara mbele ya mgeni rasmi ,Martine Lubango kwa niaba ya wahitimu wa darasa la saba matwiga wamesema kuwa pamoja na shule hiyo kuwa imala na kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa umeme, barabara, computer, printa na upungufu wa walimu.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo Katibu wa kamati ya elimu na mazingira wa Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi (CCM ) Wilaya ya Sengerema Martine Lubango ameahidi kutatua baadhi ya chanagamoto zinazoikabili shule hiyo .
Mkuu wa shule ya Sekondari Nyampulukano Mwl,Mathias Misungwi Paul ameahidi kutoa kompyuta kwa ajili ya kurahisisha katika shughuli za uchapishaji wa mitihani katika shule ya msingi matwiga.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya msingi matwiga Mwl, ,Boniphase Katalyeba amewapongeza viongozi wote walioshiriki na kutoa michango yao katika ujenzi Wa maendeleo ya shule hiyo pamoja na walimu kwa kuendelea kuendelea kujenga taaluma katika shule hiyo.