Sengerema FM

Shule ya Sekondari Katunguru yapania kuongeza ufaulu 2024

5 October 2024, 7:09 pm

Mgeni Rasmi Bwn. Martine Kimisha akizungumza kwenye mahafari ya 34 ya shule ya Sekondari Katunguru.Picha na Joyce Rollingstone

Shule ya Sekondari Katunguru ni miongoni mwa Shule Kongwe zilizopo Wilayani Sengerema na imekuwa ikifanya Vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne na cha pili mitihani ya kitaifa.

Na;Joyce Rollingstone

Shule ya Sekondari Katunguru  wilayani Sengerema mkoani Mwanza ,imejipanga kuweka mazingira bora ya kumuwezasha mwanafunzi kuongeza ufaulu kwa mithihani ya kidato cha nne.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa shule hiyo Bwn  Baraka Ezekieli Msimba  wakati akisoma risara ya shule mbele ya mgeni rasmi,ambapo amesema kuwa wanajivunia kuwa na ufaulu mzuri kwa wanafunzi kwa asilimia mia moja , na kuweka  heshima kubwa kwa shule hiyo.

Sauti mkuu wa shule hiyo Bwn  Baraka Ezekieli Msimba akielezea mafanikio ya shule hiyo

Aidha Msimba, amepongeza Mh,Rais wa jamhuli ya muungano wa Tanzania, kwa kuwapatia fedha kwa ajiri ya ujenzi wa madarasa na mwabweni kwa kidato cha tano,ikiwa ni pamoja na shule kuweka mipango madhubuti ya kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi wawapo shuleni.

Sauti mkuu wa shule hiyo Bwn  Baraka Ezekieli Msimba akielezea mikakati ya kuongeza ufaulu shuleni hapo

Naye mgeni rasimi Bwn. Martine Kimisha amewakumbusha wahitimu kuwa  jukumu lao ,ni kuendelea kujiandaa katika  mitihani yao ya taifa, ili kuweza kuendelea kuitangaza shule kitaaluma na kuwasihi kumutanguliza mungu katika masomo yao ,huku akiwataka wanafunzi wanaobaki  kuendelea  kuwa   na maadili na nidhamu .

Sauti ya mgeni Rasmi Bwn. Martine Kimisha kwenye mahafari shule ya sekondari Katunguru

Bwana kimisha hakusita  kuwakumbusha wazazi na walezi wa watoto kuwa wanawajibu wa kuwalea watoto wao, na sikuwaachia walimu pekee ikiwa ni pamoja na  kuwatimizia mahitaji ya shule.

Sauti ya mgeni Rasmi Bwn. Martine Kimisha kwenye mahafari shule ya sekondari Katunguru

Kwa upande wao wazazi wa watoto waliohudhulia mahafali hayo ,wamewaomba wazazi kuchangia michango yao kwa wakati , ambayo wamekubaliana katika vikao vya wazazi ,ili kuwawezesha watoto kusoma bila changamoto.

Sauti ya Wazazi wakizungumza namna wanavyoshilikiana na walimu shuleni hapo

Hata hivyo mgeni rasimi aliwatunuku vyeti jumula ya wanafunzi 305  wa kidato cha nne,ikiwa wasichana 150 na wavulana 155, kwenye mahafali ya 34 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo,ambapo  viongozi mbalimbali wa dini, chama na serikali, wamehudhulia mahafari hayo.

Mkuu wa shule hiyo Bwn  Baraka Ezekieli Msimba akielezea mafanikio ya shule hiyo.Picha na Joyce Rollingstone