Sengerema FM

Kipindi maalum kuelekea uchaguzi serikali za mitaa Buchosa

26 September 2024, 8:54 pm

Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Buchosa Bwn. Benson Mihayo akizungumza na Radio Sengerema kwenye kipindii maalum kuelekea uchaguzi Serkali za mitaa. Picha na Emmanuel Twimanye.

Wananchi Halmashauri ya Buchosa wametakiwa kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika November 27 mwaka huu nchini.

Hayo yamebainishwa na msimamizi wa uchaguzi halmashauri hiyo Bwn. Benson Mihayo, ambapo amesema kuwa zoezi la uchukuaji fomu za kugombea zitatolewa na kurudishwa tarehe 01 hadi 07 Novemba kwa msimamizi wa uchaguzi na kampeni zitaanza tarehe 20 hadi 26 Novemba na zitafanyika kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni.