Sengerema FM

Watakiwa kujitokeza kugombea uongozi serikali za mitaa

26 September 2024, 3:50 pm

Msimamizi  wa uchanguzi Halmashauri ya sengerema Binuru Mussa Shekidele akizungumzia matukio mbalimbali kuelekea uchaguzi.Picha na Richard Bagolele.

Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Sengerema amewataka wananchi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura, kwa ajili ya uchaguzi wa serkali za mitaa mwezi Novemba mwaka huu.

Na:Tumain John

Wananchi Halmashauri ya Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotalijiwa kufanyika November 27 mwaka huu nchini.

Hayo yamebainishwa na msimamizi  wa uchanguzi Halmashauri ya sengerema Binuru Mussa Shekidele ambapo amesema wananchi wote wenye sifa za  kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika maeneo yao kupitia vyama vyao vya siasi wanapaswa kujitokeza na kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo.

Sauti ya msimamizi  wa uchanguzi Halmashauri ya sengerema Binuru Mussa Shekidele akizungumzia sifa za wagombea uchaguzi serkali za mitaa.

Katika hatua nyingine Shekidele amesema kuwa uchanguzi utafanyika katika vitongoji husika na wakazi wenye umri kuanzia miaka 18 wanasifa za kupiga kura na kumchangua kiongozi katika eneo lao.

Sauti ya msimamizi  wa uchanguzi Halmashauri ya sengerema Binuru Mussa Shekidele akizungumzia sifa za wagombea uchaguzi serkali za mitaa.

Aidha ameongeza kua zoezi la uchukuaji fomu za kugombea zitatolewa na zinatakiwa kurudishwa tarehe 01 hadi 07 november kwa msimamizi wa uchaguzi na kapeni zitaanza tarehe 20 hadi tarehe 26 november na zitafanyika saa 2:00 asbuhi mpaka saa 12:00 jioni.

Sauti ya msimamizi  wa uchanguzi Halmashauri ya sengerema Binuru Mussa Shekidele akizungumzia sifa za wagombea uchaguzi serkali za mitaa.

Hata hivyo Zoezi la uchaguzi linatarajiwa kufanyika Jumatano ya tarehe 27 november mwaka huu ambapo wananchi wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kuchangua viongozi watakao waogoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.