Mtoto wa miaka 6 atelekezwa na baba yake mzazi mjini Sengerema
25 September 2024, 8:26 am
Kufuatia kuwepo kwa matukio ya mauaji na utekaji wa watoto nchini, baadhi ya wazazi au walezi wamekuwa na tabia ya kutelekeza watoto mtaani nyakati za usiku na baadaye kulalamika kuwa watoto wao wametekwa na wasiojulikana.
Na:Emmanuel Twimanye
Mtoto anaye kadiliwa kuwa na umri wa mika sita na mwanafunzi wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi Iyogelo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza ametelekezwa na Baba yake mzazi kwenye Daraja lililopo katika mpaka wa Mtaa wa Igogo na Misheni Wilayani hapo .
Akizungumzia tukio hilo kwa uchungu mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Balikisi Majidu amesema kuwa alitamaini kutoka katika eneo hilo ili amfuate baba yake lakini alishindwa .
Baadhi ya wananachi wa mtaa wa Igogo wamesikitishwa na tukio hilo na kuwaomba wazazi kuacha tabia ya kutelekeza watoto ili kuepuka kuhatarisha usalama wao.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Igogo Godluck Daud amethibitisha kutelekezwa kwa mtoto huyo majira ya saa moja usiku ambapo wasamalia wema walimuokota na kumpeleka nyumbani kwa kwenyekiti huku akiwataka wazazi kuwa makini na watoto wao hususani katika kipindi hiki cha matukio ya utekaji na mauaji yanayoendelea nchini.