Sengerema FM

Wastaafu waaswa kuacha kutumia ‘pensheni’ kwa anasa

14 September 2024, 3:27 pm

Meneja wa banki ya TCB Wilayani Sengerema Joseph Fumbo akizungumza na Radio Sengerema Ofisini kwake.Picha na Emmanuel Twimanye

Wasitafu wengi nchini wamekua wakijikuta wakiishi maisha magumu licha ya Serkali kuwalipa kiinua mgongo,huku baadhi yao wakitajwa kutumia pensheni zao kwa anasa za Dunia.

Na Emmanuel Twimanye.

Wazee  wastaafu wilayani  Sengerema  mkoani Mwanza wametakiwa kuacha kutumia pensheni zao kwa  anasa badala yake wazitumie kwa kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo .

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa banki ya TCB Wilayani Sengerema Joseph Fumbo  wakati akiongea na Radio Sengerema kufuatia baadhi ya wazee wilayani humo kutumia fedha hizo kwa anasa na kutesa familia zao.

Sauti ya Meneja wa banki ya TCB wilayani Sengerema Joseph Fumbo akizungumzia umuhimu wa kuwekeza kupitia Pensheni kwa wastaafu.

Aidha  Meneja huyo amesema  ili kukabiliana na  suala hilo   Benki hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa wazee wastaafu juu ya namna ya kutumia vizuri pensheni hizo.

Sauti ya Meneja wa banki ya TCB Wilayani Sengerema Joseph Fumbo akizungumzia umuhimu wa kuwekeza kupitia Pensheni kwa wastaafu.

Licha ya serikali kuwalipa pesheni wazee wastaafu lakini baadhi yao wamedaiwa kutonufaika kutokana na kutumia  vibaya pensheni hizo  ikiwemo  Anasa .