Sengerema yajipanga kuwainua wakulima msimu huu
6 September 2024, 1:40 pm
Wilaya ya Sengerema ni miongoni mwa wilaya inayozalisha chakula kwa wingi kanda ya ziwa na hujiingizia mapato mengi kupitia sekta hiyo pia imetoa ajira nyingi kwa wakazi wa wilaya hiyo kutokana na kukeza kwenye kilimo cha bustani kwani wilaya hiyo imezungukwa na ziwa Victoria.
Na;Elisha Magege
Halmashauri ya Sengerema imezindua msimu mpya wa kilimo mwaka 2024/25 huku ikijiwekea malengo ya kuvuna Zaidi ya Tani laki mbili za mazao ya chakula na biashara.
Akizungumza katika uzindduzi huo mkuu wa wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga amewataka wakulima wote wilayani hamo kupima sampuli za udogo wa mashamba yao kupitia maabala ya udogo iliyopo ofsi za kilimo ilikujua mahitaji ya mbolea inayohitajika kulingana na mazao pia kupata elimu Zaidi kutoka kwa wataalamu.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya kilimo Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Sengerema Mwita Chacha Waryuba amesema Kulingana na taarifa za mamlaka ya hali ya Hewa wamejipanga kuanza kuhamasisha kilimo mapema ili kukabiliana na hali ya uhaba wa mvua za vuli kama ilivyotangazwa na TMA.
Aidha wakulima wameishukuru Serkali kwa kuwakumbusha kuanza maandalizi ya kilimo mapema, huku wakisema uwepo wa maabala ya kupima udogo katika Halmashauri ya Sengerema itawasaidia kupunguza gharama walizokuwa wakitumia hapo awali kwenye kilimo.
Halmashauri ya Sengerema musimu uliopita ilizalisha tani 216,543 za chakula huku lengo likiwa tani 229,626 na mahitaji ya chakula kwa halmashauri yote ni tani 116,457 hivyo msimu ulipita ilibaki na ziada ya tani 100,086 ya chakula.