Sengerema FM

DED Sengerema asisitiza utoaji wa huduma bora za afya

16 July 2024, 5:08 pm

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Sengerema Binuru M.Shekidele akizungumza na wahudumu wa afya Haspitali ya Wilaya Mwabaruhi Sengerema. Picha na Richard Bagolele

Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan imewekeza fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za nchini ambapo katika Halmashauri ya Sengerema fedha nyingi zimeletwa kwa ajili ya kununua vifaa tiba na uboreshaji wa miundo mbinu.

Na:Elisha Magege

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Binuru Shekidele amewataka watoa huduma za afya vilivyopo katika Halmashauri ya Sengerema kuhakikisha wanatoa huduma bora za afya sambamba na kuzingatia usafi katika maeneo yay a kazi.

Hayo ameayabainisha wakati wa ziara ya kukagua utoaji wa huduma katika Hospitali ya Wilaya Mwabaluhi pamoja na vituo vya afya Buzilasoga na Nyamazugo ambapo amesema watumishi waliopo katika maeneo hayo wanapaswa kulinda rasilimali zote zilizopo katika vituo hivyo sambamba na itoaji wa huduma bora kwa wananchi .

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Sengerema Binuru Mussa Shekidele

Mapema akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya Nyamazugo Shekidele amemwagiza fundi anayejenga kituo hicho kukamilisha kazi hiyo kwa ubora huku akimtaka kuhakikisha dosari zote zilizipo katika baadhi ya majengo zinarekebishwa ili kituo hicho kianze kutoa huduma haraka.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Sengerema Binuru Mussa Shekidele

Aidha katika kituo cha afya Kanyerere kilichopo kata ya Buzilasoga, kinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa  Maji, ambapo mkurugenzi amesema tayali ameshazungumza na mbunge wa jimbo la Sengerema na kuahidi wiki ijayo wataanza kuchimba kisima kirefu katika kituo hicho.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Sengerema Binuru Mussa Shekidele

Hata hivyo Shekidele amemwagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Sengerema kuhakikisha zoezi la uwekaji wa njia za watembea kwa miguu ndani ya hospitali ya wilaya pamoja ufungaji wa vitanda na vifaa mhimu linapewa kipaumbele ili kuboresha upatikanaji wa huduma katika hospitali hiyo.