Sengerema FM
Sengerema FM
29 January 2026, 2:40 pm

Kundi la waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda wilaya ya Nyangh’wale wamepewa mafunzo ya usalama barabarani yenye lengo la kuwasaidia kupata lesseni za udereva na kufuata sheria za usalama barabarani.
Na,Said Mahera
Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Grace Kingalame, amefungua mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva bodaboda wanaofanya shughuli za kusafirisha abiria bila leseni za udereva.
Kingalame amesema mafunzo hayo yanalenga kuwarahisishia madereva bodaboda utaratibu wa kupata elimu ya usalama barabarani, kupata cheti cha udereva na hatimae kupata leseni za udereva.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Nyang’hwale Ndg. Husna Toni amewapongeza madereva bodaboda kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Bodaboda Wilaya ya Nyang’hwale Ndg. Julius Wiliamameishukuru Serikali kwa kuweka utaratibu mzuri wa gharama nafuu kwa madereva bodaboda kupata mafunzo ya usalama barabarani na hatimaye kutunukiwa vyeti.