Sengerema FM
Sengerema FM
23 January 2026, 7:17 pm

Wakulima katika wilaya ya Nyang’hwale wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dr. Samia Suluhu Hassani kwa kupata mbengu za Alzeti bure sambamba na Mbolea za rudhuku, zenye lengo la kumuinua mkulima nchini.
Na;Said Mahera
Mamlaka ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imetoa tani 23 za mbengu za alizeti katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita kwa ajili ya msimu mpya wa kilimo cha zao hilo.
Afisa Kilimo wa Wilaya ya Nyang’hwale, Ndg. Gudala Kija, akitoa tani 1.25 za mbegu za alizeti kwa wananchi wa Kata ya Izunya, kuelekea msimu mpya wa kilimo cha zao hilo la alizeti amesema mbegu hizo wakulima wa kata zote 15 katika halmashaurti hiyo.
Kwa upande wake Afisa Ugani wa Kata ya Izunya, Ndg. Samson Makubate, amesema kabla ya kuanza zoezi la ugawaji wa mbegu hizo, wananchi wamepatiwa elimu ya kutosha kuhusu kilimo bora cha alizeti, ikiwemo namna sahihi ya kupanda, kudhibiti wadudu waharibifu pamoja na matumizi sahihi ya mbolea.

Nao wananchi Wananchi wa Kata ya Izunya wameishukuru Serikali kwa kuwapatia mbegu za alizeti kuelekea msimu mpya wa kilimo cha zao hilo.
Hata hivyo afisa kilimo amewahimiza wakulima kutumia mbegu hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuhakikisha wanapata mavuno bora na kufanikisha juhudi za serikali za kukuza sekta ya kilimo.