Sengerema FM

TADB yawatembelea wafugajiwa samaki ziwa Victoria

14 December 2025, 6:28 pm

Baadhi ya vijana wanaojishughulisha na uvuvi wa vizimba wakiwa kwenye moja ya vizimba vya samaki katika ziwa victoria.Picha na Elisha Magege

Baada ya Serkali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kutoa fursa kwa wavuvi kuanza ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ndani ya ziwa victoria, baadhi ya wananchi katika Halmashauri ya Buchosa wamefurahishwa, na kuiomba serikali kuwaongezea ujuzi na mitaji ili waachane na uvuvi haramu ndani ya Ziwa victoria.

Na Elisha Magege

Bank ya maendeleo ya wakulima nchini TADB imevitembelea vyama vya ushirika Buchosa vinavyojihusisha na ufugaji wa samaki wa vizimba katika ziwa victoria.

Akizungumza na wandishi wa habari akiwa eneo la mradi katika kijiji cha Itumbili kata ya Nyakarilo. Bi Glacia Marugujo Afsa biashara wa Bank ya TADB, amesema mapaka sasa bank hiyo imewekeza Zaidi ya bilioni1 kwa vikundi vya ushiriki vinavyojihusisha na ufugaji wa samaki ndani ya ziwa Victoria,ambapo kwa vyama vya ushirika vya wavuvi katika  halmashauri ya Buchosa awamu ya kwanza walipewa Zaidi ya milioni 700.

Sauti ya afsa biashara wa Bank ya TADB Bi Glacia Marugujo

Kwa upande wake mwenyekiti wa vyama vya ushiriki Buchosa Bwn.Msilikale Juma Mkeju Amesema ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba u   mewapa faidi ya Zaidi ya Tsh. Mil.30 ndani ya miezi 7 kwani soko la ndani ni kubwa kuliko uzalishaji wao.

Sauti ya mwenyekiti wa vyama vya ushiriki Buchosa Bwn.Msilikale Juma Mkeju

Aidha baadhi ya wananchi wameishukuru Serikali kwa kuwekeza katika uvuvi wa vizimba kwani unasaidia kuondoa uvuvi haramu uliokuwa umekisiri katika ziwa Victoria.

Sauti za baadhi ya wananchi wanaonufaika na mradi wa samaki wa vizimba Buchosa

Hata hivyo Bank ya TADB imewataka vijana na wanawake kujiunga na kuunda vikundi vitakavyo pewa mikopo kwa ajili ya kilimo na ufugaji kote nchini.

Afsa kutoka bank ya TADB akitoa elimu kwa wanufaika wa mradi Buchosa.Picha na Elisha Magege