Sengerema FM
Sengerema FM
2 December 2025, 3:15 pm

Utoaji elimu kwa jamii juu ya maambukizi ya VVU na UKIMWI Halmashauri ya Sengerema imesaidia kupunguza kuenea kwa kasi maambukizi mapya VVU.
Na;Elisha Magege
Maabukizi ya Virusi vya ukimwi katika Halmashauri ya Sengerema Mkoani Mwanza yamepungua kutoka asilimia 2.0 mwaka 2023/24 hadi asilimia 1.8 mwaka 2025.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwa Duniani yaliyofanyika katika Kijiji cha Chifunfu, mratibu wa afua za ukimwi na magonjwa ya Gono na homa ya ini halmashauri ya Sengerema Dr.Magreth Buzoya, amesema kufuatia elimu wanayoendelea kuitoa kwa umma mambukizi yanazidi kupungua mwaka hadi mwaka.
Kwa upande wake Ndg. Mohamed Kombo, Mratibu wa kudhibiti ukimwi na afua za ukimwi ngazi ya jamii Halmashauri ya Sengerema, akizungumza kwa niaba ya mgeni Rasimi, amewataka wadau mbalimbali kuungana kwa pamoja kutoa elimu ili kudhibiti mambukizi mapya ya (VVU) katika jamii.

Aidha baadhi ya wananchi wa kijiji cha chifunfu wameishukuru Serkali ya Halmashauri ya Sengerema kwa kufanya maadhimisho hayo kwenye eneo la kijiweni, kwani wameweza kupima afya zao bure bila malipo.
Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Dunia hufanyika kila mwaka Desember mosi ambapo kwa mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu ya “Shinda vikwazo imarisha mwitikio, Tokomeza ukimwi,jitambue,Pima afya yako leo”
