Sengerema FM
Sengerema FM
27 November 2025, 3:02 pm

Matukio ya watu kuuawa kwa kukatwa mapanga wilayani Sengerema yalidhibitiwa kwa muda mrefu, jambo lililowafanya wananchi kushituka baada ya tukio la hivi karibuni kutokea katika kata ya Sima
Na,Emmanuel Twimanye
Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Kajanja Mtebi (50) mkazi wa Kijiji cha Sogoso kata ya Sima Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza ameuawa kwa kudaiwa kukatwa katwa kwa mapanga na watu wasiojulikana ,huku chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika .
Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya ndugu na majirani wa familia hiyo wamesikitishwa na tukio hilo na kuiomba serikali kufanya uchguzi ili kubaini watu wanaodaiwa kutekeleza unyama huo na kuwachukulia hatua kali za kisheria .
Mwenyekiti wa Kijiji cha Sogoso Martine Luchagula amekiri kutokea kwa tukio hilo na kutaja jina la mtu aliyefariki kuwa ni Kajanja Mtebi .
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Ngaga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini watu waliohusika na mauaji hayo na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
