Sengerema FM

Shirika la SMD lagusa maisha ya mtoto mwenye ulemavu

22 November 2025, 7:26 pm

Mtoto Baraka akiwa kwenye kitimwendo alichokabidhiwa na shirika la SMD. Picha na Joyce Rollingstone

Baadhi ya wazazi na walezi nchini wamekuwa tabia za kutowapeleka shule watoto wenye ulemavu jambo linalokemewa vikali na Serikali pamoja na asasi za kiraia

Na;Joyce Rollingstone

Wazazi na Walezi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza, wametakiwa kutowaficha watoto wenye ulemavu na badala yake wawapeleke Shule ili kupata haki ya elimu.

Kauli hiyo imetolewa na Bi Assumpta Kaganda Afisa Maendeleo ya Jamii na Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali ,wakati Shilika lisilokuwa la kiserikali la Sengerema Mshikamano on Disability SMD lililopo Wilayani Sengerema , likikabidhi baiskeli kwa mtoto Baraka Kasheka  mwenye ulemavu wa viungo anayesoma shule ya Msingi Mayuya Darasa la Pili,ambapo amesema watoto wenye ulemavu wanahaki ya kupata elimu kama watoto wengine.

Sauti ya Afsa maendeleo ya jamii Sengerema Bi Assumpta Kaganda

Akikabidhi baiskeli hiyo Mkurugenzi wa Shirika la SMD ,Bwn Gervas Titus amsema kuwa baiskeli hiyo wameitoa kwa ajili ya mtoto Baraka ili iweze kumsaidia kufika shuleni kwa wakati na kuhudhulia masomo yake.

Sauti ya Mkurugenzi wa Shirika la SMD ,Bwn Gervas Titus

Naye Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mnazi Mmoja, kijiji cha Mayuya Bwn Lauliani Zachalia, amelipongeza shirika hilo kwa kumsaidia mtoto huyo baiskeli ambapo amesema itamsaidia kufika shuleni kwa wakati.

Sauti ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mnazi Mmoja Bwn Lauliani Zachalia

Akipokea baiskeli hiyo Baba mzazi wa Mtoto huyo, Bwn Robarti Kasheka, amelishukru shirika la SMD kwa msaada huo na kuahidi kuitunza baisikeli hiyo,na kwamba itatumika kwa matumizi sahihi ya mtoto,huku akibainisha changamoto alizokuwa akipitia mtoto kabla ya msaada huo.

Sauti ya Baba mzazi wa Mtoto Baraka, Bwn Robarti Kasheka

Makabidhiano hayo yamefanyika nyumbani kwa Robart Kasheka katika kijiji cha Mayuya kata ya Tabaluka na kuhudhuliwa na Viongozi wa Serikali ya Mtaa, Afisa maendeleo pamoja na Viongozi wa Shilika hilo.

Mtoto Baraka mwenye ulemavu akiwa na wadogo zake.Picha na Joyce Rollingstone