Sengerema FM
Sengerema FM
31 July 2025, 3:34 pm

Wivu wa mapenzi umemusababishia Bwn. Bagandosa kusakwa na jeshi la polisi baada ya kumuua mwanaume anayedaiwa kuwa mchepuko wa mke wake, na kutokomea kusiko julikana.
Na;Emmanuel Twimanye
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, linamsaka Bagandosa Silas Menelo, kwa tuhuma za mauaji ya Elias Martine Mshaki (23), mkulima na mkazi wa kijiji cha Lumeya, Halmshauri ya Buchosa baada ya kumfumania nyumbani kwake akiwa na mke wake.
Tukio hilo limetokea tarehe 29.07.2025 majira ya 01:00 asuhuhi huko kijiji cha Lumeya, wilayani Sengerema ambapo mtuhumiwa alimuua Elias Martine Mshaki kwa kumpiga na kitu butu tumboni, baada ya kumfumania marehemu akiwa na mke wake aitwaye Neema Seylvester Thobias (20), kwenye nyumba yake, ndipo ulizuka ugovi baina yao na mtuhumiwa akamshambulia Elias Martine Mshaki kwa kumpiga na kitu butu na kusababishia kifo chake.
Baada ya kutekeleza mauaji hayo mtuhumiwa alimjeruhi mke wake kwa kumshambulia na kitu butu sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha kichwani.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa Bagandosa Silas Menelo na marehemu Elias Martine Mshaki, walikuwa wanakunywa pombe pamoja na baadaye marehemu alimnunulia mtuhumiwa pombe na kumuacha akiendelea kunywa na yeye kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa mpaka alipokutwa na mtuhumiwa akiwa na mke wa mtuhumiwa.
Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitaalamu na kukabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi na majeruhi anaendelea na matibabu katika hospitali ya Halmashauri ya Buchosa.
Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, kwani inadaiwa marehemu alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa mtuhumiwa.
Baadhi ya wanachi wilayani humo wameiomba serikali kumsaka na kumchukulia hatua kali za kisheria mtuhumiwa ili kukomesha matukio ya mauaji yanayotokana na watu kujichukulia sheria mkononi.