Sengerema FM
Sengerema FM
28 July 2025, 5:17 pm

Kampuni ya Nukta Afrika imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari radio za kijamii juu ya namna ya habari za uongo na upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya mitandao ya kijamii, hususa ni kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Na,Michael Mgozi
Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuhakikisha wanatoa taarifa za kweli na zenye uhakika huku jamii ikiaswa kuwa makini na habari wanazopata kupitia mitandao ya kijamii kwa kujilidhisha kabla ya kuzisambaza.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mafunzo ya siku tatu Mkoani Morogoro, Mkuu wa Mafunzo na utafiti kutoka Kampuni ya Nucta Afrika, Daniel Samson amesema mafunzo hayo yametolewa kwa waandishi wa habari wa Radio za kijamii ili kuwajengea uwezo juu ya kukabiliana na habari za uzushi na uongo na kuwawezesha kuandika habari za kweli kutoka katika vyanzo sahihi.
Aidha Samson ametoa wito kwa Waandishi kuiepusha jamii na taarifa za uongo, nakuwataka wananchi kuhakikisha wanakuwa makini pindi wanapopata taarifa kutoka katika mitandao, na kutokuzisambaza bila kujilidhisha.
Kwa upande wao waandishi waliopatiwa mafunzo, wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuandika habari za ukweli na ukakika katika kuuhabarisha umma.
Mafunzo hayo yameandaliwa kwa pamoja kwa kushilikiana na Kampuni ya Nukta afrika, na Shirika la Internation Media Suport(IMS) kwa ufadhili wa Shirika la maendeleo la Swiden(SIDA) kwa lengo la kuongeza wigo wa kupata taarifa sahihi kwa jamii zitakazosaidia kukuza maendeleo kwa wananchi.