Sengerema FM
Sengerema FM
4 June 2025, 5:37 pm

Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Sengerema na waziri wa zamani wa nishati na madini Wiliam Mganga Ngeleja ametimiza ahadi yake aliyoitoa kwenye harambee ya ujenzi Ofisi ya Kata ya Ibisabageni ya kutoa Tofari 2,000, zilizo kabidhiwa leo na Ndg.Festo Lugega.
Na;Joyce Rollingstone
Jumla ya tofari Elfu Mbili na Mia Tano zimetolewa kwa ajiri ya Ujenzi wa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kata ya Ibisabageni Mjini Sengerema Mkoani Mwanza.

Akikabidhi tofari hizo mwakirishi wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh Wiliamu Mganga Ngeleja Ndug, Lugega Festo Petro, ikiwa ni kutekeleza ahadi aliyotoa katika halambe ya ujenzi wa ofisi hiyo ya Ccm.
Sambamba na hilo, pia Lugega amewakabidhi tishert 50 wanakikundi cha Wanawake na Samia kilichopo katika kata ya ibisabageni, ikiwa ni kuunga mkono jitiahada za akina mama hao.

Naye mjumbe wa kamati ya siasa mkoa wa Mwanza Bi Elizabethi Watson Nyingi, amekabidhi mifuko 10 ya Saruji ikiwa ni kutekeleza ahadi aliyoitoa katika halambee ya ujenzi wa ofisi hiyo ,na kusema kuwa amefulahishwa na kuanza kwa ujenzi huo.
Katibu wa Ccm kata ya Ibisabageni Bwn, Barnabas Charles Butondo, amewashukuru wote waliotimiza ahadi zao, na kuahidi kutumia tofali na saruji hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Ujenzi wa ofisi hiyo utarahisisha utoa huduma kwa wanachama wa CCM kwani ofisi iliyokuwa ikitumika awali imechakaa kutokana na kutumika kwa mda mrfeu.
