Sengerema FM
Sengerema FM
3 June 2025, 3:26 pm

Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha kwa baadhi ya maeneo nchini Tanzania, mashimo na madimbwi yamejaa maji jambo linaloweza kusababisha maafa kama watoto watacheza kwenye maeneo hayo,na katika wilaya ya Sengerema mtoto mmoja amefariki baada ya kuzama kwenye dimbwi lililokuwa na maji.
Na,Emmanuel Twimanye
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aliyefahamika kwa jina la Tekela Simon amefariki Dunia baada ya kuzama kwenye dimbwi la maji katika kata ya Tabaruka ya zamani Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.
Wazazi wa mtoto huyo wamesikitishwa na tukio hilo na kueleza kuwa walikwenda shambani na kumwacha mtoto huyo na wenzake nyumbani na kwamba baada ya kurudi hawakumkuta ndipo walipoanza kumtafuta na kumkuta amezama kwenye dimbwi la maji na kupoteza maisha .
Baadhi ya ndugu na majirani wa familia hiyo wamepokea tukio hilo kwa masikitiko na kuomba wazazi kukufukia madimbwi hatarishi yaliyopo karibu na makazi yao ili kunusuru maisha ya watoto.
Mwenyekiti wa mkitongoji cha Tabaruka ya Zamani Abdallah Masasila amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananachi kuwa makini na watoto .
Kwa upande wake Jeshi la Polisi Wilaya ya Sengerema limefikia eneo la tukio na kuruhusu ndugu kufanya taratibu za mazishi.
