Sengerema FM
Sengerema FM
10 May 2025, 6:42 pm

Kufuatia kukithiri kwa ajali za barabarani nchini Chuo cha udereva cha Nyota Kilichopo jijini mwanza kimeanzisha darasa la udereva linalotembea, ambapo kimekita kambi wilaya ya Sengerema kufundisha udereva na sheria za usalama barabarani.
Na.Elisha Magege
Vijana wanao endesha vyombo vya moto wametakiwa kupata mafunzo ya udeleva kutoka vyuo vinavyotambulika kisheria ili waweze kupata leseni kwa mujibu wa sheria.
Rai hiyo imetolewa na kaimu mkuu wa usalama barabarani wilaya ya Sengerema Norshid Mussa wakati akifunga mafunzo ya udereva salama yaliyotolewa na chuo cha udereva cha Nyota kilichopo Mwanza, ambapo amaesema ili kuwa dereva bora ni lazima uwe na taaluma ya udereva itakayo kusaidia kujua sheria na taratibu za usalama barabarani.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa chuo cha Nyota Driving School Timothew Mbwambo amesema kilicho wasukuma kuanza kutoa mafunzo ya udereva maeneo mbalimbali nchini ni kutokana na kushamili kwa ajali za barabarani zinazosababishwa na uzembe na kutokujua sheria kwa madereva.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameupongeza uongozi wa chuo cha nyota Driving School kwa kufika katika wilaya ya Sengerema na kutoa mafunzo hayo, kwani wengi wao walikuwa wakiendesha pikipiki bila mafunzo jambo lililokuwa likipelekea kukamatwa mara kwa mara na trafiki.
Aidha kaimu mkuu wa usalama barabara Sengerema Norshid Mussa amewataka madereva wote ambao leseni zao zimemaliza muda kuhaikisha wanazihuisha, ambapo kwa mjibu wa sheria watatakiwa kuonyesha vyeti vya udereva au kupata mafunzo kabla ya kuzihuisha.