Sengerema FM

Avuna samaki wa vizimba vya Rais Samia Buchosa

8 April 2025, 8:54 pm

Pichani ni samaki wakitoka kuvunwa kwenye kizimba ndani ya Ziwa Victoria Halmashauri ya Buchosa.Picha na Elisha Magege

Katika kuhakiki mazingira ya uvuvi ndani ya Ziwa Victoria yanazidi kuimarika serikali ilitoa mkopo kupitia Bank ya Kilimo kwa wavuvi kuanzisha vikundi vya ufugaji wa Samaki, ambapo tayari vikundi kutoka Halmashauari ya Buchosa mkoani Mwanza vimeanza kuvuna samaki hao.

Na;Elisha Mgaege

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Buchosa Benson Mihayo ameahidi kuendelea kuboresha miundo mbinu kwa wafanya biashara wa samaki kutoka ziwa Victoria.

Mihayo ameyasema hayo alipovitembelea vyama vya ushirika vinavyo jihusisha na ufugaji wa samaki wa vizimba vilivyopatiwa mkopo na Serikali katika  kijiji cha Itumbili kata ya Nyakaliro,ambapo amesema baada ya kupokea pongezi nyingi kutoka kwa wanaushirika kuwa biashara ya ufugaji wa samaki inafaida,nakwamba serikali itaendelea kuboresha miundo mbinu kwa wafanya biashara wa samaki.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Buchosa Bwn. Benson Mihayo akizungumzia kuboresha miundo mbinu kwa wafanya biashara wa Samaki

Mkuu wa wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga amevipongeza vikundi vya ushirika kwa kufanya vizuri awamu hii ya kwanza huku akiendelea kuwasisitiza wananchi na wafanya biashara wa Samaki kuwekeza kwenye ufugaji wa Samaki na kuachana na uvuvi haramu.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga akizungumzia ufugaji wa samaki wa vizimba Buchosa

Aidha wananchi wameishukuru Serikali ya awamu ya Tano chini ya Dr. Samia, kwa kuwekeza nguvu katika ufugaji wa Samaki jambo lililowasaidia kupata vitoweo,huku wakiomba viongezwe vizimba vitakavyowezesha kuvuna samaki wakati wote.

Sauti ya baadhi ya wananchi na wafanya biashara wa Samaki Buchosa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mnamo Januari 30, 2024 alizindua Ugawaji wa Vizimba vya Kufugia Samaki 222 kwa wanufaika 1,213 na Boti za Kisasa 160 vyenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bil. 2. ambapo kwa halmashauri ya Buchosa tayari wameanza kuvuna samaki huku wakimshukuru Rais kwa miradi hiyo na kutoa fedha kwa wavuvi.