

14 March 2025, 7:44 pm
Ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi mjini Sengerema Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (SEUWASA) imekabidhi pikipiki 5 kwa watumishi wa idara ya Ufundi na huduma kwa mteja wa mamlaka hiyo.
Na,Emmanuel Twimanye
Watumishi wa Mamlaka ya maji Mjini Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kutotumia pikipiki walizopewa na serikali kinyume na matumizi ya mamlaka hiyo ikiwemo Bodaboba na uhalifu .
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji Mjini Sengerema Sadala Sadick wakati akikabidhi pikipiki kwa watumishi wa mamlaka hiyo na kuwataka kutumia pikipiki hizo kwa kazi za mamlaka hiyo na si vinginevyo.
Katika hatua nyingine Mhandisi Sadick amesema kuwa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya mjini ni asilimia 94 huku pembezoni ni asilimia 76 .
Nao baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo waliopewa pikipiki hizo wameishukuru serikali kwa kutoa usafiri huo kwa kuwa utarahisisha utendaji wao wa kazi ikiwa ni pamoja na kuwafikia wananachi kwa urahisi tofauti na hapo awali.