Sengerema FM
Sengerema FM
28 February 2025, 6:46 pm

Waganga wa kienyeji wamekua na tabia ya kufanya mapenzi na wagonjwa wao jambo ambalo limepingwa na viongozi wa chama wa CHAWATIATA kuwa nii kosa na si maadili ya kazi hiyo.
Na,Emmanuel Twimanye
Wagaga wa tiba asili Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wameonywa kuacha mara moja tabia ya kufanya ngono na wagonjwa pindi wanapokwenda kupata huduma za matibabu .
Onyo hilo limetolewa na mwenyekiti wa chama cha waganga na wakunga wa tiba asili mkoani Mwanza Shabani Ramadhani katika kikao cha waganga wa tiba asili kilichofanyika wilayani Sengerema .
Mwakilishi kutoka ofisi ya mkuu wa upelelezi na makosa ya jinai wilayani Sengerema Inspekta Athumani Waziri amekiri kupokea malalamiko ya kulalamikiwa baadhi ya waganga kufanya ngono na wagonjwa na kuwataka waganga kuachana na vitendo hivyo.
Nao baadhi ya waganga wa tiba asili waliohudhuria kikao hicho wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria waganga watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo kwa kuwa wanachafua kazi hiyo.