

4 February 2025, 7:08 pm
Kuelekea maadhimisho ya miaka 48 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) viongozi wa chama hicho maeneo mbalimbali nchini wamefanya matukio tofautitofauti ikiwemo kukagua miradi ya maendeleo na matendo ya hisani kama vile kuchangia damu na kufanya usafi mahospitalini.
Na; Jovna George
Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilayani Sengerema amemuagiza afisa mtendaji wa kata ya Chifunfu kuhakikisha anawachukulia hatua kali wazazi ambao wameshindwa kuwapeleka watoto shuleni.
Hayo yamejili mara baada ya kubainika kuwa zaidi ya wanafunzi 129 bado hawajaripoti katika shule ya Sekondari Bungumbikiso iliyopo kata ya Chifunfu Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza waliochanguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule hiyo.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Ccm Wilayani Sengerema Bi Waridi Josephat ametoa maagizo hayo wakati wa kufanya ukaguzi wa miradi 3 ndani ya kata ya chifufu katika kuelekea sherehe ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa chama hicho na kusema kuwa kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi ambao hawajalipoti shule iko haja ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya wazazi na walezi ili kuhakikisha wanalipoti kabla ya Februari 8 mwaka huu.
Awali akisoma taarifa mkuu wa Sekondari Bugumbikiso mwl Shadrack shing’oma mbele ya katibu wa chama cha mapinduzi ccm wilayani sengerema amesema katika shule hiyo jumla ya wanafunzi 288 walipangiwa kuripoti na hadi sasa waliolipoti ni wanafunzi 169 huku akieleza wananfunzi wengine 30 wamepewa uhamisho wa kuhamia shule ya Sekondari Chifufu.
Katika hatua nyingine katibu wa ccm wilaya amekagua kituo cha afya cha Ngomamtimba na kubaini changamoto zilizopo katika kituo na kuahidi serikali ya ccm kuzifanyia kazi.
Jumla ya miradi 3 ya kata ya Chifufu imekaguliwa na katibu wa chama cha mapinduzi ccm ikiwa ni kuelekea katika sherehe ya kuzaliwa kwa chama cha hicho.