Sengerema FM

Chuo kikuu cha Ardhi kampasi ya Mwanza kujengwa Sengerema

4 February 2025, 12:33 pm

Makamu mkuu wa Chuo kikuu Ardhi Prof.Evaristo Liwa Akikabidhi ramani za majengo yatakayo jengwa katika eneo la ujenzi wa chuo hicho Kampasi ya Sengerema Mwanza Kwa Mhandisi Hasheem Ibrahim Lema Mkurugenzi kampuni ya Comflix Engenering Ltd .Picha na Elisha Magege

Ujenzi wa chuo kikuu cha Ardhi Kampasi ya Mwanza unatarajia kuanza kutekelezwa kuanzia February 17 mwaka huu katika kijiji cha Karumo wilayani Sengerema,Ukigharimu kiasi cha Tsh. Bil.16.3.

Na;Elisha Magege

Wananchi wilayani Sengerema mkoani Mwanza wametakiwa kutoa ushirikiano kwa mkandarasi wa ujenzi wa chuo kikuu Ardhi kampasi ya Sengerema Mwanza, inayo jengwa kijiji cha karumo kata ya Nyamatongo wilayani hapo.

Rai hiyo imetolewa na Mh. Enock Sengerema kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema katika hafla ya kukabidhi eneo kwa mkandarasi aliyeshinda tenda ya ujenzi kampuni ya Comflix Engenering Ltd, ambapo amesema wananchi wa maeneo yanayo zunguka mradi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kulinda laslimali zote zitakazo tumika kwenye ujenzi huo.

Sauti ya Mh. Enock Sengerem diwani kata ya Nyamazugo akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti Halmashauri ya Sengerema Mh. Yanga Makaga

Naye Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Ardhi  Profesa Evaristo Liwa amesema, kampasi hiyo inajengwa kupitia mradi wa mageuzi ya kiuchumi kupitia elimu ya Juu (HEET) hivyo amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa mradi huo kwa wakati huku akiwashukuru wananchi wa kata ya Nyamatongo kwa kukubali kupisha ujenzi wa chuo hicho na Halmshauri ya Sengerema kusimamia  vyema zoezi la uthamini wa eneo la mradi huo.

Sauti ya Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Ardhi  Profesa Evaristo Liwa akizungumzia mradi wa ujenzi wa chuo kikuu Ardhi kampasi ya Mwanza

Aidha kaimu mkurugenzi Halmashauari ya Sengerema Dr.Davison Adrew pamoja na wananachi wameushukuru uongozi wa chuo kikuu Ardhi kwa uamzi wa kureta mradi huo Sengerema.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema Dr. Davison Adrew na wananchi wakizungumzia ujenzi wa chuo hicho.

Ujenzi wa chuo hicho kwa awamu ya kwanza utaanza na majengo matano ambayo  madarasa, jengo la utawala, mabweni ya wanafunzi, jengo la walimu pamoja na Zahanati kwa gharama ya shilingi bilioni 16 na milioni 300 ujenzi utafanyika kwa muda wa miezi 15 na chuo hicho kikikamilika kwa awamu ya kwanza kitakuwa na uwezo wa kudahili wanachuo zaidi ya 2,000 kwa ngazi ya shahada, sitashahada na cheti.