Askofu Malasusa asifu ushirikiano wa KKKT na Halmashauri ya Sengerema
22 January 2025, 7:06 pm
Mradi wa USAID Kizazi Hodari Wilaya ya Sengerema ulianza mwezi Oktoba 2023, lengo la mradi huo ni kuboresha huduma za afya, ustawi, ulinzi na usalama kwa watoto walio katika mazingira hatarishi kata ya Igulumuki mradi huo umeweza kutoa huduma kwa walengwa 77
Na;Deborah Maisa
Askofu mkuu wa kanisa la kinjili la kilutheri Tanzania KKKT Alex Malasusa amesema madhehebu ya dini yataendelea kushirikiana na serikali katika katika kudumisha Amani.
Askofu Malasusa ameyasema hayo wakati wa ziara yake wilayani sengerema mkoani mwanza kwa lengo la kuangalia shughuli zinazofanywa na mradi wa USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kaskazin Mashariki katika kata ya igulumuki ambao upo chini yakanisa la KKKT nchini.
Mkurugenzi wa halmashauri ya sengerema Binuru Shekidele amemshukuru Askofu Malasusa kwa mradi huo katika kata ya igulumuki ambapo amesema kupitia mradi huo walengwa wanaweza kujiinua kiuchumi.
Akisoma taarifa kwa askofu malasusa katibu wa kikundi cha umoja Igulumuki Yunis Zacharia amesema kikundi kianzishwa mwaka 2022 kikiwa na wanachama 23 ambao wote ni wanawake kupitia kikundi hicho wameweza kuwafungulia watoto watatu bima ya Afya kwa ajili ya matibabu.
Afisa ustawi wa jamii halmashauri ya Sengerema Nyanjige Julius amesema mradi wa USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kaskazin Mashariki ulipokealewa katika wilaya ya sengerema October,2023 na mradi huo umewafikia walengwa 4992.