Sengerema FM

Wenyeviti wa Vijiji warudishwa darasani kusoma uongozi

12 January 2025, 2:12 pm

Mkufunzi Bwn,Jonas Kabwadi akitoa elimu kwa wenyeviti wa vijiji na vitoongoji Halmashauri yya Sengerema.Picha na Elisha Magege

Kupitia uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika nchini November 24 mwaka jana 2024 viongozi waliochaguliwa kwa nafasi zao, leo wamepewa mafunzo ya namna ya kuweza kuongoza vijiji na mitaa bila kuingiliia maslahi ya watendaji wa vijiji na kata.

Na;Elisha Magege

Viongozi wa Serikali za mitaa vijiji na vitongoji Halmashauri ya Sengerema wametakiwa kutambua mipaka ya kazi wanapotekeleza majukumu yao.

Rai hiyo imetolewa na Bwn.Jonas Kabwandi Mkufunzi kutoka chuo cha uongozi serikali za mitaa Hombolo Dodoma wakati akitoa  mafunzo kwa viongozi wa Serkali vijiji na vitongoji  Halmashauri ya Sengerema ambapo amesema kupitia mafunzo haya viongozi hao watatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba ya nchi.

Sauti ya Mkifunzi Mr.Jonas Kabwadi akizungumzia mafunzo aliyoyatoa kwa viongozi serkali za mitaa Sengerema

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Halmasahuri ya Sengerema Mkuu wa idara ya mazingira Ally Salim amewataka wenyeviti hao kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia waliyoelekezwa kwenye mafunzo.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema Bwn,Ally Salim akizungumuzia Mafunzo yaliyotolewa kwa wenyeviti

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Serkali ya Jamhuri ya Muungano kwa kuwaletea mafunzo hayo huku wakiahidi kwenda kutekeleza majukumu yao kwa vitendo.

Sauti za Washiriki wa mafunzo ya uongozi serkali za mitaa Sengerema

Halmashauri ya Sengerema ina jumla ya vijiji 71, vitongoji 421 kutoka tarafa 3, Ambapo walio patiwa mafunzo ya uongozi Serikali za mitaa ni wenyeviti wa vijiji,vitongoji na wajumbe wa serkali za mitaa.