Prof. Lyaya atoa msaada kwa wagonjwa Mwanza
24 December 2024, 9:50 pm
Katika kuelekea sikukuu za mwisho wa Mwaka watu mbalimbali hujitolea misaada kwa wahitaji kama sehemu ya ibaada na kumbukumbu kwa jamii inayo wazunguka.
Na;Elisha Magege
Jamii imetakiwa kujitoa na kusaidia wenye uhitaji wakiwemo wagonjwa, wafungwa na wenye mahitaji maalumu hasa kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
Rai hiyo imetolewa na Prof.Edwinus Chrisantus Lyaya Prof.mshiriki wa Sayansi ya Ikolojia kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Baada ya kwenda kuwatembelea wagonjwa mbalimbali katika kituo cha Afya Kisesa wilayani Magu, nakutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa hao.
Aidha Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Kisesa Dr. Pauline S.Karoli amemshukuru Prof. Lyaya kwa kufika kituoni hapo na kutoa msaada kwa wagonjwa, huku akitoa wito kwa wengine kuendelea kusaidia wenye uhitaji.
Baadhi ya Wagonjwa na viongozi mbalimbali wamemshukuru Prof. Lyaya kwa kutoa msaada huo, kwani kuna wagonjwa wengine walikuwa hawana msaada, hivyo kwa alichokitoa kitawasaidia kwa kipindi hiki.
Kituo cha afya Kisesa ni miongozni mwa vituo 7 vya afya vilivyopo wilaya ya Magu na kinatoa huduma mbalimbali wa tarafa ya Sanjo na kata ya Bujora na kisesa, na kinakadiliwa kuhudumia Zaidi ya wagonjwa 5000 kwa mwezi.