Sengerema FM

Sengerema imepanda miti 500 kumbuukumbu ya miaka 63 ya uhuru

9 December 2024, 2:42 pm

Wananchi na viongozi wakipanda miti. piccha na Elisha Magege

Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 kutoka kwa mkoloni mwingereza, ikikabbidhiwa kwa mwl. julius K.Nyerere akiwa kama waziri mkuu wa kwanza mtanganyika na badae rais wa kwanza wa taifa hilo,na leo imetimia miaka 63 tangu kupatikana kwa uhuru huo.

Na;;Elisha Magege

Halmashauri ya Sengerema imeadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania bara kwa kupanda miti na kufanya usafi maeneo mbalimbali ya kijamii.

Akiongoza zoezi la upandaji miti katika eneo la shule ya Sekondari mpya Isungang’holo Katibu tawala wilaya ya Sengerema Curthbert Midala, amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kupanda miti kwani inafaida nyingi ikiwemo kutunza mazingira.

Sauti ya Katibu tawala wilaya ya Sengerema Curthbert Midala akizungumziaa faida za upandaji miti

Kwa upande wake Afsa mazingira Halmashauri ya Sengerema Bi.Tandy Laizer amesema jumla ya miti 500 imepandwa katika eneo la ujenzi wa shule ya Sekondari isungang’holo ikiwemo miti ya matunda,mbao na vivulli.

Sautii ya Afsa mazingira Halmashauri ya Sengerema Bi.Tandy Laizer akizungumzia miti iliyopandwa leo

Naye Kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema Bwn. Wilbert Bandola  amewashukuru wananchi kujitokeza kuazimisha miaka 63 ya uhuru kwa kupanda miti eneo hilo.

Sauti ya Kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema Bwn.Wilbert Bandola akiendellea kuhimmiza wananchi kupanda miti

Aidha Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isungang’holo Bwn.Michael Sumuni pamoja na wananchi wamewashukuru viongozi wa halmashauri ya Sengerema kwa kuteua eneo hilo kupanda miti huku wakiahadi kuitunza.

Sauti za wananchi na viongozi kitongoji ccha Isunganng’holo

Hata hivyo wakala wa huduma za misitu Tanzaniaa (TFS) wilaya ya Sengerema inatoa miche ya miti bure kwa wananchi, lengo likiwa ni kupanda miti kwa kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema Bwn.Fredrick Mugarula akizungumza na wananchi waliojitokeza kupanda miti Isungang’holo.Picha na Elisha Magege
Katibu Tawala wilaya ya Sengerema Bwn.Curthbert Midala akizungumza na wananchi waliojitokeza kupanda miti eneo la Isungang’holo.Picha na Ellisha Magege
Moja ya wananchi waaliojitokeza kupaanda miti kumbukumbu ya miaka 63 ya uhuru Picha na Elisha Magege