FDC Sengerema yakabiliwa na uhaba wa vifaa vya kufundishia
6 November 2024, 11:34 am
Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sengerema (FDC) kilianzishwa Mwaka 1978 lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi kupata ujuzi wa fani mbalimbali ili kukabiliana na changamoto ya ajira nchini.
Na;Joyce Rollingstone
Chuo cha Maendeleo ya Wananchi FDC kilichopo Wilayani Sengerema,kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemi ukosefu wa Mashine yenye uwezo wa kushona viatu aina zote.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa chuo hicho Bi Monika Rukeha,wakati akisoma risala ya chuo mbele ya Mgeni Rasimi na kusema kuwa chuo hicho kinakabiliwa na ukosefu wa mashine ya kushonea bidhaa za ngozi huku akitaja mafanikio yaliyofikiwa na chuo hicho.
Aidha bi Rukeha hakusita kuwaasa wahitimu wa chuo hicho kutumia ufundi walioupata katika chuo hicho, na kuwaomba kufanya kazi kwa bidii na nidhamu.
Naye Mgeni Rasimi Bwan, Japhet Samwel Kiboya,ameanza kwa kuwashukuru wahitimu na kuwatia moyo kwa kuweza kukabiliana na mapungufu yaliyopo hapo chuoni ,na kuweza kukabiliyana nayo,na kuwaomba wakatumie vizuri ufundi walioupata chuoni na si kukaa kusubili ajira.
Nao wazazi waliohudhulia katika mahafari hiyo wamewapongeza walimu kwa kazi nzuri, pamoja na kutoa wito kwa wazazi kuwaruhusu watoto kwenda kutumia ujuzi walioupata na si kukaa nyumbani na kusubili ajira,bali wajiajiri wakiwa wanasubili ajira.
Hata hivyo Mgeni Rasimi amepata flusa ya kuwatunuku vyeti wahitimu 229 wakike 57 na wakiume 172 kwa fani mbalimbali katika mahafali ya 25 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho na na viongozi wa chama na serikali,pamoja na wazazi.