Isangi filam Tanzania wampongeza DC Sengerema kwa kutambua mchango wao
24 October 2024, 3:47 pm
Isangi films Tanzania kikundi cha vijana wilayani Sengerema kilicho amua kutoa elimu mbalimbali kwa jamii kupitia sanaa ya maigizo, Huku kikijitanabaisha kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.
Na:Joyce Rollingstone
Wasanii wa Isangi filam Tanzania, Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza ,Wametakiwa kuheshimiana pamoja na kuwa wamoja ,ikiwa ni pamoja na kuilinda Amani ya Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kikundi cha Sanaa cha Isangi Filam Tanzania, Bwan Hojas Walles wakati akiongea na wasanii mbalimbali wa kikundi hicho ,na kusema kuwa Wasanii wanatakiwa kutambua kuwa wao ni kioo cha jamii,hivyo hawana budi kiilinda Amani iliyopo, ikiwa ni pamoja kukemea mambo ambayo yanasababisha mmomonyoko wa maadili ,pamoja na kupiga vita madaya ya kulevya.
Aidha Walles amewaomba wasanii kuendelea kushilikiana na ofisi za Selikari na Taasisi mbalimbali,ikiwa ni mipango madhubuti waliyojiwekea katika kuboresha Miundombinu katika jamii ,ambapo wamejipanga kufanya usafi ,kuzibua daraja zilizoziba na kazi hiyo itaanza pindi tu vitendea kazi watakapovipata .
Walles hakusita kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe; Senyi Saimon Ngaga ,kwa kutambua uwepo wa wasanii wa Isangi Filam Tanzania,kwa kutambua mchango wao katika jamii.
Nao baadhi ya wasanii wa kikundi hicho ,wamesema kuwa wamepokea maelekezo hayo na kuahidi kuwa watakuwa bega kwa bega na kiongozi wao, kutekeleza yale yote walioadhimia katika vikao vyao ,ikiwa ni pamoja na kufanya Sanaa wakizingatia mavazi yanayofaa katika jamii.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Busega complex na kuhudhuliwa na wasanii mbalimbali wa nyimbo na filam.