Sengerema FM

Tabasamu ashirikiana na wananchi kujenga daraja

15 October 2024, 6:48 pm

Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh,Hamis Tabasam akishirikiana na wananchi kuchanganya zenge kwa ajili ya ujenzi wa Daraja.Picha na Emmanuel Twimanye

Wananchi wa kijiji cha Butonga wilayani Sengerema wafurahia serkali ya awamu ya sita chini ya Dr.Samia kwa kuanza ujenzi wa daraja lililokuwa likisababisha vifo kwao kwa muda mrefu.

Na;Emmanuel Twimanye

Daraja   lililokuwa  likihatarisha  maisha ya wananchi    katika Kijiji cha Butonga kata ya  Igulumuki  Wilayani Sengerema  Mkoani Mwanza    limeanza kujengwa na Serikali ili kunusuru maisha ya wakazi wa Kijiji hicho.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Sengerema kwa kusimamia ujenzi wa daraja hilo kwa kuwa litakapokamilika litawasaidia kuokoa maisha ya wananachi.

Sauti za wananchi wakizungumzia ujenzi wa Daraja la kijijini kwao

Naye Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh,Hamis Tabasam ameridhiwa na ujenzi wa daraja hilo pamoja na ujenzi wa barabara ya yenye urefu wa Kilomita  53 kutoka Sengerema hadi mizolozolo na kuipongeza serikali kwa ujenzi huo .

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh,Hamis Tabasam akizungumzia ujenzi wa daraja

Ujenzi wa daraja hilo linagharimu kiasi cha Tsh.180 na unatarajia kukamilika mwezi November 30 mwaka huu.

Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh,Hamis Tabasam akizungumza na wananchi wakichanganya zenge kwa ajili ya ujenzi wa Daraja.Picha na Emmanuel Twimanye