Mavunde awatuliza wananchi mgodi wa Sota Sengerema
13 October 2024, 12:01 pm
Mgodi wa dhahabu wa SOTA GOLD Mining uliopo kata ya Igalula wilayani Sengerema mkoani Mwanza unatarajiwa kuanza uzalishaji mwakani 2025, ambapo kwasasa wameaanza madalizi ya ujenzi wa Mgodi huo,ikiwemo kuwahamisha wananchi wenye maeneo yanayo pakana na eneo la mgodi huo.
Na;Emmanuel Twimanye
Wananachi Waliopisha Mgodi wa Sotta uliopo katika Kijiji cha Sota kata ya Igalula Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wameiomba Serikali kuingilia kati suala la kujengewa nyumba sambamba na wazawa kupewa kipaumbele cha ajira katika mgodi huo.
Wananchi hao wametoa ombi hilo mbele ya wazairi wa madini Mh,Anton Mavunde katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ngoma.
Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh, Hamis Tabasam amewaomba viongozi wa kampuni hiyo ya mgodi kuhakikisha wanajenga nyumba za wanufaika haraka huku akimuomba waziri kuhakikisha mgodo huo unatenga eneo ala wachimbaji wadogo.
Afisa Mkuu wa Fedha na kaimu meneja wa Mgodi wa Sota Isack Lupokela amesema kuwa tayari wakandarasi wamekwisha patikana kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo pamoja na kuahidi kulipa kipaumbele suala la ajira kwa wazawa.
Naye Waziri wa Madini Mh,Anton Mavunde amemwagiza Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Nganga kuhakikisha anasimamia zoezi la ajira kikamilifu ili wazazwa waweze kunufaika na mgodi huo.