VTC Sengerema yaendelea kuzalisha vijana wenye ujuzi nchini
12 October 2024, 4:39 pm
Serkali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewekeza fedha nyingi kujenga vyuo vya ufundi nchini ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa ajira kwa vijana, waweze kujiajiri kupitia ufundi.
Na;Deborah Maisa
Wahitimu wa chuo cha ufundi Sengerema vtc wametakiwa kusoma kwa bidii pindi wanapojiandaa kufanya mhihani wa kuhitimu elimu ngazi ya chuo
Wito huo umetolewa na mgeni rasmi Mchungaji Adam Malindi kwenye mahafari ya tano tangu kuanzishwa kwa chuo hicho na kuwaeleza wahitimu hao ili waweze kufaulu mitihani yao lazima wazingatie yale waliyofundishwa darasani.
Nae mkuu wa chuo cha ufundi Sengerema vtc Yela Aloyce Malando ameishukuru Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwakuanzisha chuo cha ufundi sengerema ambacho kimewawezesha watoto wa kitanzania kujiunga na chuo hicho na kupata ujuzi wa fani mbalimbali.
Nao baadhi ya wahitimu wa chuo hicho kwaupande wao wamesema ujuzi walioupata utawawezesha kujiajiri wenyewe na kuajiliwa katika makampuni ndani na nje ya nchi.
Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa rais Dr. Samia Suluhu Hasan umekuwa ikijenga vyuo vya ufundi veta kila wilaya ili kuhakikisha kila mtoto anapata ujuzi.