Shule ya Sekondari Katunguru yapania kuongeza ufaulu 2024
5 October 2024, 7:09 pm
Shule ya Sekondari Katunguru ni miongoni mwa Shule Kongwe zilizopo Wilayani Sengerema na imekuwa ikifanya Vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne na cha pili mitihani ya kitaifa.
Na;Joyce Rollingstone
Shule ya Sekondari Katunguru wilayani Sengerema mkoani Mwanza ,imejipanga kuweka mazingira bora ya kumuwezasha mwanafunzi kuongeza ufaulu kwa mithihani ya kidato cha nne.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa shule hiyo Bwn Baraka Ezekieli Msimba wakati akisoma risara ya shule mbele ya mgeni rasmi,ambapo amesema kuwa wanajivunia kuwa na ufaulu mzuri kwa wanafunzi kwa asilimia mia moja , na kuweka heshima kubwa kwa shule hiyo.
Aidha Msimba, amepongeza Mh,Rais wa jamhuli ya muungano wa Tanzania, kwa kuwapatia fedha kwa ajiri ya ujenzi wa madarasa na mwabweni kwa kidato cha tano,ikiwa ni pamoja na shule kuweka mipango madhubuti ya kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi wawapo shuleni.
Naye mgeni rasimi Bwn. Martine Kimisha amewakumbusha wahitimu kuwa jukumu lao ,ni kuendelea kujiandaa katika mitihani yao ya taifa, ili kuweza kuendelea kuitangaza shule kitaaluma na kuwasihi kumutanguliza mungu katika masomo yao ,huku akiwataka wanafunzi wanaobaki kuendelea kuwa na maadili na nidhamu .
Bwana kimisha hakusita kuwakumbusha wazazi na walezi wa watoto kuwa wanawajibu wa kuwalea watoto wao, na sikuwaachia walimu pekee ikiwa ni pamoja na kuwatimizia mahitaji ya shule.
Kwa upande wao wazazi wa watoto waliohudhulia mahafali hayo ,wamewaomba wazazi kuchangia michango yao kwa wakati , ambayo wamekubaliana katika vikao vya wazazi ,ili kuwawezesha watoto kusoma bila changamoto.
Hata hivyo mgeni rasimi aliwatunuku vyeti jumula ya wanafunzi 305 wa kidato cha nne,ikiwa wasichana 150 na wavulana 155, kwenye mahafali ya 34 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo,ambapo viongozi mbalimbali wa dini, chama na serikali, wamehudhulia mahafari hayo.