Sengerema FM

Mtoto wa miaka 6 atelekezwa na baba yake mzazi mjini Sengerema

25 September 2024, 8:26 am

Mtoto Balikisi Majidu aliyetelekezwa na baba yake usiku mjini Sengerema.Picha na Emmanuel Twimanye

Kufuatia kuwepo kwa matukio ya mauaji na utekaji wa watoto nchini, baadhi ya wazazi au walezi wamekuwa na tabia ya kutelekeza watoto mtaani nyakati za usiku na baadaye kulalamika kuwa watoto wao wametekwa na wasiojulikana.

Na:Emmanuel Twimanye

Mtoto anaye kadiliwa kuwa na umri wa mika sita na mwanafunzi wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi Iyogelo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza  ametelekezwa na Baba yake  mzazi kwenye Daraja lililopo katika mpaka wa Mtaa wa Igogo na Misheni Wilayani hapo .

Akizungumzia tukio hilo  kwa uchungu   mtoto huyo  aliyefahamika kwa jina la Balikisi Majidu amesema  kuwa alitamaini  kutoka  katika eneo hilo ili amfuate baba yake lakini alishindwa .

Sauti ya mtoto akizungumzia hali ilivyokua

Baadhi ya wananachi wa mtaa wa Igogo wamesikitishwa na tukio hilo na kuwaomba wazazi kuacha tabia ya kutelekeza watoto ili kuepuka kuhatarisha usalama wao.

Sauti ya baadhi ya wananchi mtaa wa Igogo Sengerema wakizungumzia tukio hilo

Mwenyekiti wa Mtaa wa Igogo Godluck Daud amethibitisha kutelekezwa kwa mtoto huyo majira ya saa moja usiku ambapo wasamalia wema walimuokota na kumpeleka nyumbani kwa kwenyekiti huku akiwataka wazazi kuwa makini na watoto wao hususani katika kipindi hiki cha matukio ya utekaji na mauaji yanayoendelea nchini.

Sauti ya mwenyekiti wa Mtaa wa Igogo Godluck Daud akizungumzia mkasa huo.