Wastaafu waaswa kuacha kutumia ‘pensheni’ kwa anasa
14 September 2024, 3:27 pm
Wasitafu wengi nchini wamekua wakijikuta wakiishi maisha magumu licha ya Serkali kuwalipa kiinua mgongo,huku baadhi yao wakitajwa kutumia pensheni zao kwa anasa za Dunia.
Na Emmanuel Twimanye.
Wazee wastaafu wilayani Sengerema mkoani Mwanza wametakiwa kuacha kutumia pensheni zao kwa anasa badala yake wazitumie kwa kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo .
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa banki ya TCB Wilayani Sengerema Joseph Fumbo wakati akiongea na Radio Sengerema kufuatia baadhi ya wazee wilayani humo kutumia fedha hizo kwa anasa na kutesa familia zao.
Aidha Meneja huyo amesema ili kukabiliana na suala hilo Benki hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa wazee wastaafu juu ya namna ya kutumia vizuri pensheni hizo.
Licha ya serikali kuwalipa pesheni wazee wastaafu lakini baadhi yao wamedaiwa kutonufaika kutokana na kutumia vibaya pensheni hizo ikiwemo Anasa .