Sengerema kuboresha mazingira ya wafugaji 2025
12 September 2024, 3:27 pm
Halmashauri ya Sengerema inakadiliwa kuwa na jumla ya Mifugo 108,758 ambapo mifugo hii huchangia kwenye pato la mtu mmoja mmoja pia kuzalisha maligafi za viwandani na ajira kwa wananchi wilayani hapo.
Na;Elisha Magege
Halmashauri ya Sengerema imezindua kampeni ya uogeshaji na chanjo kwa mifugo msimu wa 2024/25 huku ikitarajia kuchanja na kuogesha mifugo zaidi ya laki moja.
Akitoa taarifa fupi kwa mkuu wa wilaya ya Sengerema ambeye ndie alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo, Bwn.Ezekiel D.Mbwana afsa mifugo kata ya Kahumumlo amesema katika kuhakikisha sekta ya mifugo inaleta tija wamejipanga kutoa elimu wezeshi kwa wafugaji.
Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga amesema ili tuwe na ufugaji wenye tija ni vyema wafugaji wakapewa elimu juu ya ufugaji wa kisasa na umhimu wa kutibu mifugo yao.
Nao baadhi ya wafugaji wilayani hapo wameipongeza serkali ya jamhuli ya muungano wa Tanzania kwa kuwawezesha wataalamu wa mifugo kila kata huku wakipogeza jitihada za idara hiyo wilayani Sengerema.
Hata hivyo baadhi ya viongozi walio ambatana na mkuu wa wilaya katibu wa mbunge Alex Maduka na Diwani wa kata ya Kahumulo Mh. Fortunatus Nzwagi wameishukuru Serikali kwa uamzi wa kutoa elimu kwa wafugaji juu ya ufugani wenye tija.
Uzinduzi huo umefanyika kijiji cha Kahumulo kata ya Kahumulo Wilayani Sengerema ambapo zaidi ya mifugo 200 imeogeshwa na kupata chanjo.