Polisi watoa msaada kituo cha watoto yatima Sengerema
8 September 2024, 2:34 pm
Katika kuadhimisha kutimiza miaka 105 ya Jeshi la Polisi Tanzania, jeshi hilo limejipanga kutoa elimu na msaada kwa jamii .
Na;Elisha Magege
Jeshi la polisi wilayani Sengerema limetoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha bustani ya watoto Misheni Sengerema kama sehemu ya maazimisho ya kutimiza miaka 105 ya jeshi hilo nchini Tanzania.
Akikabidhi msaada huo mkuu wa upelelezi wilayani Sengerema ASP.Tito Mohe amesema jeshi hilo katika kuazimisha miaka 105 tangu kuanzishwa kwake, limejipanga kutoa elimu na misaada mbalimbali kwa jamii kama sehemu ya majukumu ya jeshi hilo.
Kwa upande wake mlezi wa kituo hicho Dr. Sister Marry Josee amelishukuru jeshi la polisi kwa kuendelea kuwatembelea kituoni hapo na kutoa msaada huo huku akiomba pia wadau mbalimbali kuendelea kusaidia kwani kituo hicho kinaendeshwa kwa misaada ya wananchi.
Kwa niaba ya mkuu wa kituo cha polisi Sengerema Inspector Grandino Chang’a Pamoja na mkuu wa operation Sengerema wamewaasa vijana kuacha mara moja kujihusisha na makundi maovu katika jamii.
Hata hivyo watoto katika bustani hiyo wamelishukuru jeshi la polisi kwa msaada huo .