Sengerema FM

Mwenyekiti ajitosa kulima barabara kwa mkono-Geita road

31 July 2024, 7:54 pm

Mwenyekiti wa Geita Road Bwn.Pelana Bagume akilima moja ya barabara ya mtaa huo.Picha na Emmanuel Twimanye

Mwenyekiti wa mtaa wa Geita Road Kata ya Nyatukala Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza  Bwn, Pelana Bagume amehudumu kwa takribani mihula minne akiwa kiongozi wa mtaa huo na wananchi wameendelea kumuamini kutoka na utendaji kazi wake.

Na;Emmanuel Twimanye

Mwenyekiti wa mtaa wa Geita Road Kata ya Nyatukala Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza  Bwn, Pelana Bagume amelazimika kukarabati   baadhi ya barabara za mtaa kwa kutumia  jembe la mkono   ili  kuwaondolea usumbufu  wananchi.

Akizungumza na Radio Sengerema baada ya zoezi la kukarabati barabara hizo amesema kuwa amelazimika kukarabati barabara kwa kutumia jembe la mkono baada ya kuona wananachi wanateseka kupita katika barabara hizo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Geita road Bwn, Pelana Bagume akizungumzia jinsi anavyojitelea kwa wananchi

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amewashauri viongozi wengine kuwatumikia wananachi kwa vitendo  ikiwa ni pamoja na kujitolea katika shughuli za maendeleo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Geita road Bwn, Pelana Bagume akiwahimiza wananchi kujitolea kufanya kazi za kijamii

Nao baadhi ya wananachi wa mtaa huo wamempongeza mwenyekiti kwa kujitolea kukarabati barabara hizo.

Sauti ya wananchi wakizungumza namna mwenyekiti wao anavyojitolea