Sengerema FM

Jamii yatakiwa kuwa makini na mawakala wa ajira nje ya nchi

30 July 2024, 3:27 pm

Picha kwa msaada wa mtandao wa x wa UN

Tarehe 30 Julai,na mara zote kila mwaka huwa ni Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, uhalifu wa kutisha na mashambulizi kamili dhidi ya haki, usalama na utu wa binadamu.

Na:Elisha Magege

Ili kukabiliana na wimbi la usafirishaji haramu wa Binadamu, Jamii imetakiwa kuwa makini na watu wanaojiita mawakala wa ajira nje ya nchi na kuepukana na tamaa ya mafanikio ya haraka.

Rai hiyo imetolewa na Stephano Mahozi John Mchambuzi wa masuala ya kijamii Nchini katika kipindi cha Safari Mseto Radio Sengerema, ambapo amesema ulimwengu wa sasa umekuwa na ushawishi mwingi kupitia mitandao hivyo ni vyema kuchunguza kwanza kupitia tasisi zinazohusika kama ubarozi wa nchi husika.

Sauti ya Mchambuzi wa masuala ya kijamii Stephano Mahozi John

Aidha Mahozi amesema baadhi ya vyonzo vinavyosababish kuendelea kuwepo kwa usafirisha haramu wa binadamu dunia ni uwepo wa vita na tamaa za kupata mafanikio kwa uharaka.

Sauti ya Mchambuzi wa masuala ya kijamii Stephano Mahozi John

Kila inapofika tar 30 mwezi wa saba kila mwaka Dunia huazimisha siku ya kupinga usafirisha haramu wa binadamu Duniani ambayo iliasisiwa na Umoja wa mataifa UN kupitia mkutano wake mkuu mwaka 2013.