Sengerema FM

Mbunge awataka wananchi kujitokeza kujiandikisha kupiga kura

20 July 2024, 6:28 pm

Mbunge wa Jimbo la Busanda Mhandisi Tumaini Magesa akihutubia wananchi kuhusu kujiandikisha na kubooresha taarifa za kwenye daftari la mpiga kura.Picha na ofsi yaa mbunge

Mbunge wa jimbo la Busanda amekuwa na mwendelezo wa kufanya mikutano ya hadhara kwenye jimbo lake yenye lengo la kusikiliza kero kutoka kwa wananchi.

Na;Elisha Magege

Mbunge wa Jimbo la Busanda Mhandisi Tumaini Magesa amewaomba wananchi wote wa Jimbo hilo kwenda kujiandisha na kuboresha taarifa kwenye daftari la kuduma la kupiga kura.

Magesa amesema hayoo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Nyaruyeye ulikua na lengo la kusikiriza kero kutoka kwa wananchi wa jimbo hilo.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Busanda Mhandisi Tumaini Magesa akizungmza na wananchi wa kata ya Nyarruyeye kuhusu kujiandikisha

Aidha Magesa amesema kujiandikisha kutasaidia kupunguza malalamiko kwa mtu, na  itampa uhuru wa kuamua kumpa ama kutokumpa kura kwenye Uchaguzi ujao.

Wananchi wa kijiji cha Nyaruyeye wakimsiikiliza mbunge kwenye mkutanno wa hadhara wa mbunge huuyo.