Waziri Nape aitaka jamii kutumia vizuri mitandao
18 July 2024, 8:07 pm
Mkoa wa Mwanza inajengwa minara 50 ya mawasiliano na mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF itayowanufaisha zaidi ya wakazi 885,420 wa vijijini.
Na: Elisha Magege
Waziri wa Habari Mawasiliano na teknolojia Nape Nauye amewataka wazazi na walezi nchini kuwafundisha vijana maadili ya kitanzania na si kuwaacha wajifunze kwenye mitandao ya kijamii.
Waziri Nape ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara wilayani Sengerema ambapo amesema nivyema wazazi wakawafundisha mila na desturi za kiafrika ili kuepukana na matukio ya udhalilishaji yanayotokea kwenye mitandao ya kijamii Duniani.
Katika hatua nyingine Waziri Nape amesema serikali ya Dr. Samia inajenga minara 750 nchii nzima ili kuwasaidia wananchi wa vijijini kupata huduma za mawasiliano.
Naye Mbunge wa Sengerema Mh. Hamis Tabasam amemshukuru waziri Nape kwa kufika huku akiomba wizara yake kuvisaidia baadhi ya vijiji vilivyopo Sengerema, ambavyo havina mitandao ya mawasiliiano ya uhakika.
Waziri Nape amefanya ziara ya kikazi mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Sengerema yenye lengo la kufuatilia upatikanaji wa mawasiliano vijijini na kutembelea mnara wa simu uliojengwa kwa ubia na serkali katika kisiwa cha Lyakanyasi Kata ya Chifunfu wilayani Sengerema.