Watakaotumia vyandarua kufugia vifaranga, bustani kukiona
10 July 2024, 3:00 pm
Mkoa wa Mwanza umepokea vyandarua Milioni 1.4 kwenda Halmashauri 6 vitagawiwa kwa wananchi bila malipo zikilenga kaya zote ambazo zinakabiliwa na changamoto ya ugonjwa Maralia
Na:Elisha Magege
Katika jitihada za kupambana na ugonjwa wa maralia nchini Halmashauri ya Sengerema inatarajia kungawa bure vyandarua vyenye dawa zaidi ya laki 2.
Hayo yamesemwa na Bwn. Abdurahman Mgonja mratibu wa malaria Sengerema ambapo ameitaka jamii kutumia vyandarua hivyo katika matumizi sahihi yaliyokusudiwa na serikali kwa kutoa vyandarua hivyo.
Katika hatua nyingine mgonja amesema jamii imekuwa na dhana potofu kuwa vyandarua vyenye dawa vinavyotolewa na Serkali husababisha madhara kwa watumiaji ikiwepo kueneza kunguni na kupunguza nguvu za kiume kwa akina baba jambo ambalo siyo kweli.
Aidha Mgonja amesema serkali haitasita kuwachukulia hatua wale watakao tumia vyandarua hivyo kufugia kuku au kwenye bustani za bongabonga.