Jamii yatakiwa kuwa mstari wa mbele kuwalinda wenye ualbino
9 July 2024, 1:29 pm
Serikali kupitia kwa waziri mkuu Kassimu Majaliwa akiwa Bungeni Dodoma hivi karibuni alisema Serkali inaandaa Mpango wa Kuzuia Ukatili dhidi ya Watu wenye Ualbino (NAP) kwa kushirikiana na Chama cha Watu Wenye Ualbino (TAS) na wadau
Na:Elisha Magege
Jamii imetakiwa kuwa mstari wa mbele kuwalinda watu wenye ualbino ili waishi kwa amani hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.
Rai hiyo imetolewa na Sheikh Mikidad Ally Lwamakobo kwa niaba ya Sheikh wa wilaya ya Sengerema kwenye kipindi cha Safari Mseto ambapo amesema jamii inatakiwa kumrudia mwenyezi Mungu kwani matukio haya yamekuwa yakitokea hata ndani ya Familia za watoto wenye ualbino.
Kwa upande wake Mratibu wa waganga wa Tiba Asili Halmashauri ya Sengerema Bwn. Deogratias Madalu amesema Serkali kwa kushirikiana na jeshi la Polis mkoa wa Mwanza limeanza kufanya msako wa kuwabaini waganga wanao fanya lamuli chonganishi na kuwakamata.
Aidha jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Kupitia taarifa aliyoitoa kwa wandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Wilbroad Mutafungwa amesema jeshi hilo linawashikilia waganga wa jadi 63 kwa tuhuma za kufanya lamuli chonganishi.