Sengerema FM

50/50 yatajwa kuwa chanzo cha migogoro ya ndoa

19 June 2024, 1:34 pm

Mwanasaikolojia Stephano Mahozi John akizungumza kwenye kipindi cha safari mseto Radio Sengerema.Picha na Elisha Magege

Suala la 50 kwa 50 limekua chanzo cha migogoro mingi kutokana na baadhi ya wanandoa kuhisi kuwa wanaweza fanya kitu chochote ambacho mwenza wake anafanya.

Na:Elisha Magege

Jamii imetakiwa kutambua maana ya neno 50 kwa 50 kati ya mwanamke na mwanaume ili kuondoa changamoto ya migogoro katika ndoa.

Hayo yamesemwa na mwanasaikolojia Stephano Mahozi John katika kipindi cha safari mseto cha Radio Sengerema ambapo amesema watu wengi katika jamii hawana uelewa waa neno 50 kwa 50 ndio maana ndoa nyingi zimekua na migogoro siku hizi.

Sauti ya mwanasaikolojia Stephano Mahozi John akifafanua maana ya 50 kwa 50

Katika hatua nyingine Mahozi amesema ni vyema mwanaume akabaki kuwa kiongozi katika familia pia asimame katika majukumu yake ya kutatua kila changamoto katika familia.

Sauti ya mwanasaikolojia Stephano Mahozi John akitoa ushauri kwa wanandoa kuhusu 50 kwa 50

Hata hivyo kwa mjibu wa kifungu cha 9 cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 Ndoa maana yake ni muungano wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke unaokusudiwa kudumu kwa muda wa maisha yao yote.