Sengerema FM

Wenye ualbino wahakikishiwa ulinzi na jeshi la polisi Mwanza

24 May 2024, 8:09 pm

Mratibu wa Polisi jamii Mkoa wa Mwanza  Jovitha  Tibangayuka Akizungumza na wazazi na walezi wa watoto wenye ualbino na watendaji wa kata Sengerema. Picha na Emmanuel Twimanye

Licha ya jeshi la polisi kuendelea kutoa elimu na kukemea vitendo vya uhalifu nchini baado lindi la biasharra za viungo vya binadamu hasa wenye ulemavu wa Ngozi linaaendelea kutokea hasa kwa mikoa ya kanda ya Ziwa.

Na;Emmanuel Twimanye

Jeshi la Polisi Mkoani  Mwanza   limewagiza    maafisa  watendaji wa kata Wilayani Sengerema kuanzisha ulinzi shirikishi katika kata zao ili kuimarisha   ulinzi dhidi ya  watu  wenye ualbino.

Agizo hilo limetolewa na Mratibu wa Polisi jamii Mkoa wa Mwanza  Jovitha  Tibangayuka  kwa niaba ya Kamanda wa polisi Mkoani mwanza Wilbroad Mtafungwa katika kikao cha kujadili mikakati ya kuimarisha ulinzi dhidi ya watu wenye  ualbino kilichofanyika Wilayani Sengerema, huku akikemea waganga wa tiba asili wanaopiga ramli chonganishi .

Sauti ya Mratibu wa Polisi jamii Mkoa wa Mwanza  Jovitha  Tibangayuka

Baadhi ya maafisa watendaji  wa kata wamelipongeza jeshi la polisi kwa mikakati hiyo na kuahidi kwenda kutekeleza suala hilo ili kuimarisha ulinzi wa kundi hilo.

Sauti za Watendaji wa kata wakilipongeza jeshi la polis Mwanza kwa mkakati huo

Nao baadhi ya watu wenye   albinism  wameiomba serikali kuendelea kuimarisha ulinzi dhidi yao ili kunusuru maisha yao.

Sauti za baadhi yya watu wenye albinism na walezi wao

Aidha hivi karibuni  mtoto mwenye  ualbino  mwenye umri wa miaka 10 anayesoma Darasa la nne  shule ya msingi maalumu Katoro  Mkoani Geita  amenusurika kifo  baada ya kudaiwa kushambuliwa na mtu asiyefahamika  kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali  sehemu za kichwa na mkono .