Mitishamba chanzo cha vifo vitokanavyo na uzazi Sengerema
14 March 2024, 3:51 pm
Vifo vitokanavyo na uzazi wilayani Sengerema vimekuwa vikitajwa kuongezeka kutokana na mwitikio mdogo wa akinamama wajawazito kuhudhuria kliniki kwa wakati na matumizi ya dawa za kienyeji.
Na:Elisha Magege
Matumizi ya dawa za kienyeji yatajwa kuwa chanzo cha vifo vya akinamama wajawazito katika halmashauri ya Sengerema mkoani mwanza.
Hayo yameelezwa na Bi.Marry Mgoa mratibu wa afya ya mama na mtoto Halmashauri ya Sengerema kwenye kipindi cha safari mseto kinachorushwa na Radio Sengerema, ambapo amesema takwimu zinaonyesha ni asilimia 37 pekee ya akinamama waliohudhulia kiliniki kwa kipindi cha kuanzia mwezi January mwaka huu 2024.
Katika hatua nyingine amesema mama mjamzito anapowahi kituo cha kutolea huduma za afya akiwa na mwenzi wake hupewa ushauri na vipimo vya magonjwa mbalimbali yanayoweza kumdhuru mtoto akiwa tumboni.
Hata hivyo Halmashauri ya Sengerema imetajwa kuwa ya pili katika mkoa wa Mwanza kwa vifo vya akinamama wajawazito ikitanguliwa na halmashauri ya Nyamagana.